Header Ads

Migodi, Viwanda Vinavyoharibu Mazingira Vichukuliwe Hatua Kali - Makamu Wa Rais

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiongea na wananchi (hawapo pichani) katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani leo Butiama.

Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.
Butiama. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa viwanda na migodi inayofanya shughuli zake za uzalishaji kwa kuharibu mazingira ikiwamo utitirishaji wa kemikali  katika makazi ya watu.
Makamu wa Rais Samia Suluhu akiongea na mjane wa Rais wa Kwanza wa Tanzania Baba wa Taifa Julius Kambarage, Mama Maria Nyerere (kulia).
Amesema  kufanya hivyo kunahatarisha usalama wa wananchi na viumbe hai wengine.
Mama Suluhu Hassan ametoa agizo hilo Juni 4, kijijini Butiama mkoani Mara wakati akihutubia wananchi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.
Amesema uharibifu wa mazingira ukiachwa uendee nchini ni hatari kwa usalama wa maisha na viumbe na hivyo ni muhimu kwa viongozi katika ngazi zote kuchukua hatua zitakazosaidia kukabiliana na vitendo hivyo.

“Kutozingatia hifadhi ya mazingira kunaweza kusababisha kuparaganyika kwa mfumo wa ikolojia  na kufanya maisha yetu na ya vizazi vijavyo kuwa mashakani,” amesema
Aliongeza kuwa katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani viongozi wanapaswa kuchukua hatua za kuelimisha wananchi na kuwahamasisha ili kila mtu ashiriki katika juhudi za kuwa na uchumi unaozingatia hifadhi ya mazingira.

No comments