Header Ads

Mimi sio shabiki wa Shilole, nampenda Rosa Ree – Gigy Money

Video Vixen, Gigy Money amefunguka na kusema yeye sio shabiki wa msanii wa Bongo Fleva Shilole na wala hajawahi kufikiria kumshirikisha katika muziki ambao anafanya kwa sasa.

Akipiga stori na kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM, Gigy Money alieleza kuwa kati ya wasanii wa kike anaowakubali katika Bongo Fleva ni Rapper Rosa Ree.

“Sina hata mpango wala sitaki, sio fun wake (Shilole), labda Rosa Ree, tatizo la watu walio up wanasumbua, so hip hop its better, mimi ningepata mtu wa kuniandikia niwe nachana ningependa, I don’t love this kind of music ambayo nafanya, nafanya ili nipate hela, mimi napenda hip hop,” alisema Gigy Money.

No comments