Header Ads

MKE MDOGO WA MZEE YUSUF AZIKWA KISUTU NA MAMIA


 
MAMIA ya waombolezaji leo wamemzika marehemu Chiku Hamisi aliyekuwa mke wa mwimbaji taarab aliyestaafu na kumrudia Muumba wake, Ustaadhi Mzee Yusuf.  Chiku aliyezikwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar leo mchana, alifariki dunia katika Hospitali ya Amana jijini Dar Jumamosi  jioni ambapo alikwenda kujifungua.
Chiku alipoteza maisha akisaidiwa na wauguzi kujifungua kwa njia ya upasuaji ambapo  mwanaye aliyekuwa tumboni alifariki pia.
Shughuli za msiba na mazishi zilianzia nyumbani hapo Kariakoo Mtaa wa Amani na Livingstone ambapo mwili  ulitolewa nyumbani hapo na kwenda kuswaliwa kwenye msikiti wa Manyema.
Baada ya suala mwili ulipelekwa makaburi ya Kisutu jijini hapa.
Katika mazishi hayo Mzee Yusuf alishindwa kuzungumza chochote baada ya kuishiwa nguvu ambapo aliondolewa makaburini hapo kwa msaada wa waombolezaji.
Na Richard Bukos/GPLNo comments