Header Ads

Morata Afunga Ndoa Italia Akiwaniwa na Man U, AC Milan

Alvaro Morata akiwa na bibi harusi wake, Alice Campello, jana jijini Venice.
MCHEZA soka wa Real Madrid, Alvaro Morata, ambaye anawaniwa vikali na klabu za Manchester United na AC Milan, jana alimwoa mchumba wake, Alice Campello, huko Venice, Italia.
Mora na Alice wakionyesha penzi lao.
Morata mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na Madrid akitokea Juventus, anasemekana hana uelewano mzuri na kocha wake, Zinedine Zidane.  Hata hivyo, ndoa yake iliyofanyika katika kanisa la Basilica de Redentore iliwasahaulisha watu wengi uvumi wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania kuhusu kuihama klabu yake ya sasa.Shamrashamra za harusi ya Morata na Alice.

No comments