Header Ads

Nisha Adai Kuwa Mpenzi Wake wa sasa ni Mbwa, Awachefua Marafiki zake

Msanii wa filamu, Salma Jabu ‘Nisha’.
WAKATI waumini wa Dini ya Kiislam wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, msanii wa filamu, Salma Jabu ‘Nisha’ ametoa kali ya mwaka kufuatia kukiri kuwa na uhusiano na mbwa.

Nisha alifanya hivyo juzikati baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa amevaa gauni jeupe la harusi huku mkononi akiwa ameshika mkanda wa mbwa na kuandika kuwa, mnyama huyo ndiye mpenzi wake, jambo ambalo liliwachefua baadhi ya marafiki zake.

“Dada acha kukufuru halafu huu ni Mwezi Mtukufu, Kiislam mbwa ni najisi halafu wewe ni Muislam unashika mbwa na kusema ndiyo mpenzi wako, tangu lini mbwa akawa na uhusiano na binadamu?” aliandika mmoja wa mashabiki aliyeonekana kukerwa na kitendo hicho. Jitihada za kumtafuta Nisha kuzungumzia kitendo alichokifanya hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutopokelewa na hata alipotumiwa SMS hakujibu.

No comments