Header Ads

Okwi aibana Simba, ataka Waweke110m Mezani Atue MsimbaziEmmanuel Okwi (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Zacharia Hans Pope
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, amewataka viongozi wa Simba kama wanahitaji saini yake, waweke milioni 110 mezani ili aweze kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu. 

Simba imekuwa katika mazungumzo ya muda mrefu na Mganda huyo kwa ajili ya kumrejesha kwa mara nyingine kufuatia awali kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa.
Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe, alitua Uganda kwa shughuli zake binafsi lakini akatumia fursa hiyo kuweka mambo sawa juu ya Okwi ili asaini mkataba.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata kutoka ndani ya uongozi wa Simba, Okwi ameomba apatiwe kiasi cha shilingi milioni 110 ili aweze kuanguka wino.

“Mwenyekiti wa kamati ya usajili Hans Poppe alikuwa Uganda kuzungumza na Okwi ambapo moja ya vitu alivyovihitaji mchezaji huyo ni kuona anapatiwa dau la milioni 110 ili aweze kusaini mkataba mpya ikiwa ni pamoja na nyumba ya kuishi.
“Viongozi wanaendelea kufanya tathmini na mazungumzo yanaendelea, iwapo tutafikia makubaliano, ataingia mkataba,” alisema bosi huyo.

Alipoulizwa juu ya hilo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully, alisema: “Nawaomba wanachama na mashabiki wa Simba wawe na subira. Kwa sasa hakuna chochote kinachoendelea juu ya Okwi. Kama kuna taarifa itatolewa, lakini sasa watu wawe na subira.”

No comments