Header Ads

Pam D hafikirii kubadilisha mtindo wa nywele


 Staa wa Bongo Fleva, Pamela Daffa 'Pam D' ameamua kuongea ya moyoni baada ya watu wengi kuzungumza kuhusu mtindo wake wa nywele. Pam ameiambia Dizzim Online kuwa hafikirii kabisa kuachana na mtindo huo.
 “Yaani watu wengi wanazungumzia style yangu ya nywele, kwanini Pam D kaweka style hii muda mrefu. Labda kitu nachoweza kusema ni kwamba huwezi ukamzungumzia Pam D bila kuwa na muonekano wake wa kipekee wa nywele. Na najua kuna wengine inawakera.

 Lakini tujiulize wale ambao wanafuga dread vipi? Kwasababu ni muda mrefu pia wana dread, halafu mi naweka tofauti tofauti. Lakini lazima niwe na nywele nyekundu na sifikirii kubadilisha,” amesisitiza.
Aidha amewaomba mashabiki zake waendelee kuisupport ngoma yake, Daffa.

No comments