Header Ads

Rais wa Tff Malinzi na Katibu Wake Watiwa Mbaroni na TAKUKURURais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikirikia na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kupelekwa Polisi kwa ajili ya uchunguzi dhidi yao kwa tuhuma za rushwa.

Hilo limethibitisha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba ambaye amesema taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao, kwa sasa ifahamike kuwa viongozi hao wanawashikilia.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Malinzi na Mwesigwa walipelekwa Sentro jana na leo asubuhi wamepelekwa Makao Makuu ya Takukuru kwa ajili ya uchunguzi kwa tuhuma zinazowakabili.

No comments