Header Ads

Real Madrid Mabingwa Ulaya, Waweka Rekodi Mpya Ikiipiga Juventus Bao 4-1


Staa wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameiongoza timu yake ya Real Madrid kuweka historia barani Ulaya baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa
Ulaya kwa kuifunga Juventus.
Real Madrid imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutwaa ubingwa huo mara mbili mfululizo tangu kuanzishwa kwa mfumo mpya wa michuano hiyo
mwanzoni mwa miaka ya 1990.
Ronaldo amefunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Juventus maarufu kama Kibibi Kizee cha Turin kwenye uwanja wa Millenium jijini Cardiff nchini Wales.No comments