Header Ads

R.O.M.A Ahama Na Kijiji Cha Bodaboda Mbagala


Roma akiongea na waandishi wa habari kwamba ataandika historia mpya siku ya Idd Mosi atakapofanya shoo ya kufa mtu Dar Live ambapo amehimiza kwamba shoo hiyo si ya kukosa.
SIKU zikiwa zimeyoyoma kuelekea Sikukuu ya Idd Mosi, mkali wa Michano Bongo, Ibrahim Musa ‘R.O.M.A Mkatoliki’ amehama na kijiji cha bodaboda zaidi ya 50 pande za MbagalaZakhem jijini Dar es Salaam na kukipeleka sheli kujaza mafuta bure ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki wake waliokuwa pamoja katika kipindi alichopata matatizo.Snura akitoa ahadi yake ya kufanya manjonjo zaidi ya yale aliyoyafanya kwenye wimbo wake wa Chura.
Muda mfupi kabla ya tukio hilo, mashabiki wengi waliojitokeza wakiwemo bodaboda walipata kumsikia R.O.M.A kwa mara ya kwanza akizungumza nao baada ya kupona majeraha yaliyotokana na kutekwa huku akiwaahidi kufanya shoo ya kihistoria katika Usiku wa Nishushe Dar Live utakaofanyika Sikukuu ya Idd Mosi.Madereva wa Bodaboda wakielekea katika kituo cha mafuta kuwekewa mafuta ya bure na Roma Mkatoliki.
Akizungumza na Championi Jumamosi, R.O.M.A alisema anajua bodaboda wengi watatumika katika kuwaleta mashabiki na kuwarudisha hivyo ameamua kujitolea kila mmoja kumpatia mafuta lita mbili ikiwa ni sehemu ya shukrani zake. Kuhusiana na shoo atakayokamua Sikukuu ya Idd Mosi, R.O.M.A alisema, amejiandaa vya kutosha na kuwaomba mashabiki wote kujitokeza kwa wingi kumshuhudia akidondosha sapraizi mpya kabisa.
Roma akianza kuwawekea mafuta madereva wa Bodaboda
“Kwa muda mrefu sijafanya shoo tangu nipate matatizo hapa kati. Mara ya mwisho nilifanya shoo Dar Live nikiwa na Darassa ilikuwa Usiku wa Michano (Mkesha wa Mwaka Mpya) na waliofika waliona na ambao hawakufika walisimuliwa.
Safari hii nisingependa ikupite hii,” alisema R.O.M.A. Akizungumzia shoo hiyo, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Juma Mbizo alisema mbali na uwepo wa R.O.M.A, siku hiyo jukwaa litashambuliwa na vichwa hatari kwenye Muziki wa Hip Hop Bongo kama vile Mr. Blue, Stamina na Darassa huku mwanamama anayekimbiza kunako Muziki wa Mduara, Snura akifanya yake kwa staili ya chura.…Akiendelea kuwawekea mafuta.
Darassa
“Wengi mnajua kuwa baada ya mwaka jana Darassa kuwadatisha na Muziki kwa mara ya kwanza Dar Live, safari hii anatua kivingine akiwa na ngoma nyingine kabisaa ya Hasara Roho ambayo nayo ni amshaamsha,” alisema Mbizo.
stamina
Stamina Kuhusiana na Stamina, Mbizo alisema kuwa, siku zote ‘battle’ zake jukwaa huwa linaongea hivyo mashabiki wajipange kushuhudia vitu vyake. “Kwa michano, Stamina anajulikana, siku hiyo atatua akiwa na ngoma zake kibao akifanya battle na wakali kama Darassa na R.O.M.A tena kwa kutumia biti tofautitofauti,” alisema Mbizo.
Mr. Blue
“Wanamuita Byser au mzee wa Baki Na Mimi! Naye si wa kusimuliwa sana kuhusiana na shughuli yake awapo jukwaani. Blue ataliamsha dude na ngoma zake zote kali kama Pesa, Mboga Saba, Baki Na Mimi na nyingine kibao. Muhimu mashabiki mjitokeze kumuona Byser mpya najua mnajua muziki wake upoje.”
Snura
“Mwanamama pekee katika Muziki wa Mduara atakayelipamba jukwaa siku hiyo atakuwepo kuwaimbia na kuwaonyesha live staili ya kucheza nyimbo zake zote kali kuanzia Ushaharibu, Majanga, Chura, Najidabua, Shindu hadi wa sasa huu wa Nionee Wivu alioimba na Yamoto Band.”
Zanzibar Stars
Mbizo alizungumzia pia Kundi la Zanzibar Stars kuwa siku hiyo litazaliwa upyaaa Dar Live. “Wapenda Muziki wa Mwambao hii si ya kukosa kwani mtashuhudia vibao vipya kabisaa kutoka kwa wakali wengi wakiwemo Bi. Mwanahawa, Jokha Kassim, Mosi Suleiman na Zubeda Mlamali.
Watoto sasa
“Watoto hatujawasahau, pazia la burudani litafunguliwa mapema kuanzia saa 2:00 asubuhi ambapo mkali wa vichekesho, Bambo atawafungulia kwa kuwavunja mbavu huku wakali wa sarakasi, Wakali Dancers pamoja na wanamuziki wa Asili, Makhirikhiri kutoka Tanzania wakifanya yao,” alisema Mbizo.
Mtonyo je?
“Kiingilio kwa wakubwa ni Sh 7,000 na watoto Sh 3,000 tu na bonasi ndani yake ya kuteleza, kubembea, kupanda ndege, kuogelea na vingine vingi bureeee,” alimaliza Mbizo.

No comments