Header Ads

Roma, Snura na Stamina ‘Wamwaga’ Mafuta Kwa Bodaboda

Kutoka kushoto ni msanii Snura,Roma na Stamina wakiongea jambo kabla ya kuanza kuzungumzia shoo yao kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Uwanja wa Zakhem-Mbagala itakayofanyika Idd Mosi kwenye Ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem, Dar es Salaam.
Roma akiongea na waandishi wa habari kwamba ataandika historia mpya siku ya Idd Mosi atakapofanya shoo ya kufa mtu Dar Live ambapo amehimiza kwamba shoo hiyo si ya kukosa.
Meneja wa Ukumbi wa Burdani wa Dar Live, Juma Mbizo (kushoto) akimpa maelekezo Roma Mkatoliki.
Snura akitoa ahadi yake ya kufanya manjonjo zaidi ya yale aliyoyafanya kwenye wimbo wake wa Chura.
 
Msanii Stamina (kulia) akiongea na waandishi wa habari na wananchi waliofika uwanjani hapo kuhusu 'maraha' atakayowapa wote watakaofika ukumbi wa Dar Live siku ya Idd Mosi.

Madereva wa Bodaboda wakielekea katika kituo cha mafuta kuwekewa mafuta ya bure na Roma Mkatoliki.
...Msafara wa Bodaboda ukizidi kuongezeka wakati wa kuelekea kituo cha mafuta.
Roma akiongea na Bodaboda kabla ya kuwawekea mafuta ambapo aliwaeleza utaratibu ambao ungetumika.
Roma akianza kuwawekea mafuta madereva wa Bodaboda.
...Akiendelea kuwawekea mafuta.

Umati wa madereva wa Bodaboda wakisubiri kuwekewa mafuta na Roma Mkatoliki.
IBRAHIM Musa ambaye ni maarufu zaidi kama Roma, mkali wa Hip Hop aliyetengeneza vichwa vikubwa vya habari miezi michache iliyopita kufuatia tukio la kutekwa, leo mchana amewamwagia mafuta waendesha bodaboda katika eneo la Mbagala baada ya kutoa lita mbili kwa vijana 50!
Roma alikuwa ameambatana na wasanii wenzake wawili, Snura na Stamina, ambao watafanya shoo pamoja katika Ukumbi wa Dar Live siku ya Iddi Mosi ambapo waliongea na waandishi wa habari kuhusu jinsi watakavyotoa burudani siku hiyo.
Hafla hiyo na waandishi wa habari ilifanyika katika Uwanja wa Zakhem-Mbagala jijini Dar es Salaam.
Roma alitamba kwamba atawabeba mashabiki zake na kuwafikisha salama katika shoo hiyo.
Msanii huyo maarufu ambaye shoo hiyo itakuwa ni ya kwanza  toka apatwe na janga hilo, alisema licha ya mafuta hayo, pia siku hiyo atakuwa na ‘surprise’ kibao kwa mashabiki wote watakaojitokeza ukumbini hapo, kwani shoo hiyo ni ya muhimu sana kwake.
“Naomba nianze surprise zangu kwa kuwawekea mafuta baadhi ya rafiki zangu 50 wa bodaboda, kwani hawa ndiyo nguzo kubwa kwangu siku hiyo ya Iddi Mosi.
“Wao ndiyo watakaobeba baadhi ya mashabiki zangu kuwaleta kwenye shoo na kuwarudisha makwao salama.
“Shoo hiyo itakuwa ya aina yake kwa sababu nikiwa jukwaani nitakuwa nimezungukwa na mastaa wenzangu kama Stamina, Snura ambao mnawaona hapa, lakini ukiachana na hawa kutakuwa na Darassa, pia utapata fursa ya kusikia kidogo vionjo vya mwambao kutoka kwa Zanzibar Star na Mr Blue kwa bei ya shilingi 7,000 tu.
“Naomba kutumia muda huu kuwakaribisha wale wote wapenda burudani kwani waje wakijua kwamba siku hiyo ya Iddi Mosi burudani itakuwa sehemu moja tu hapa Dar es Salaam, na mahali sahihi ni Dar Live, hapo ndiyo utakutana na wakali wa michano wenye uwezo wa kila aina,” alisema.


No comments