Header Ads

Sabby Ajutia Picha Zake Za za nusu utupu kwani sasa amebadilika

Msanii wa filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’.
MAJUTO! Msanii wa filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amedai kuwa anajutia maisha yake ya awali ya kupiga picha za nusu utupu kwani sasa amebadilika na kujikita kwenye kumtumikia Mungu.

Akipiga stori na 3 Tamu, Sabby alisema huko nyuma alikuwa na kasumba ya kupiga picha ambazo ziko kinyume na maadili lakini sasa hivi ameacha mambo hayo ila kila akiziona kwenye mitandao anaumia sana.
“Namshukuru Mungu kwa kunifanya nibadilike, kwa sasa sina mpango tena wa kupiga picha ambazo ziko kinyume na maadili zile nilizopiga kipindi cha nyuma nimezifuta kwenye kurasa zangu mtandaoni, nimeona ni muda muafaka wa kubadilika,” alisema Sabby.

No comments