Header Ads

Shabiki Wa Yanga, Ally Yanga Afariki Dunia Kwenye Ajali Ya Gari

Shabiki mkubwa wa Yanga, Ally Yanga.
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza shabiki mkubwa wa Yanga, Ally Yanga amefariki dunia.
Taarifa zinaeleza, Ally Yanga amefariki dunia katika ajali ya gari huko Mpwapwa mkoani Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amethibitisha kwamba ajali hiyo imetokea leo mchana na Ally amepoteza maisha.
Ally Yanga anakumbukwa kutokana na mbwembwe zake kila Yanga ilipokuwa inacheza.
Alipenda kujipaka masizi meusi huku akiweka kitambi cha bandia.

Mbali na kuisapoti Yanga, alikuwa ni shabiki mkubwa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ambapo mara kadhaa alisafiri na timu kwa ajili ya kwenda kuishangilia, pia katika michezo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar alikuwa akiongoza maelfu ya mashabiki kuwaunga mkono Taifa Stars.

No comments