Header Ads

Toni Braxton Afunguka Mahusiano Yake Na Birdman

Msanii wa muziki wa R&B Toni Braxton akiwa pamoja na Boss wa Cash Money Bryan Williams “Birdman”.
STORI: SAMSON JEREMIAH / GPL
MSANII wa muziki wa R&B Toni Braxton ameweka wazi mahusiano yake kwa mara ya kwanza na Boss wa Cash Money Bryan Williams “Birdman”.
Toni Braxton amefunguka zaidi na kusema kuwa mahusiano yake na Birdman ni ya kimapenzi ila hataki kuwa na amani wala furaha katika mahusiano yao kwa sababu bado mapema na hajui kitakachofuata kati yao.
Toni anasema sababu ya kuwa muoga wa kuingia katika dimbwi la mapenzi kwa mara nyingine ni kutokana na kuwa ‘single’ kwa muda mrefu pia anaogopa kuumizwa tena.


Toni amekuwa ‘single’ toka walivyotengana na mume wake, Keri Lewis, mwaka 2009, ambapo talaka ilikamilika mwaka 2013. Wawili hao walibahatika kupata watoto wawili Denim na Diezel.
Toni na Birdman walionekana wakiwa pamoja katika tuzo za BET mwaka jana na kuzua gumzo juu ya mahusiano yao.

No comments