Header Ads

Ulinzi kabambe Ndondo Cup

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi nchini limewahakikishia ulinzi wa kutosha mashabiki watakaojitokeza viwanjani kushuhudia mashindano ya soka ya Ndondo Cup yatakayoanza rasmi Juni 17 jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yanahusisha timu za mitaani za soka kutoka maeneo mbalimbali ya jijini.
Kamishina msaidizi wa jeshi la Polisi, Phillip Karangi alisema kuwa kwa kipindi chote ambacho mashindano hayo yatafanyika kutokana na umuhimu wake kwa jamii wataweka ulinzi imara ndani na nje ya viwanja.
Mkurugenzi wa mashindano hayo, Shaffih Dauda alilishukuru Jeshi la Polisi kwa ushirikiano waliotoa kwa mashindano hayo.

No comments