Header Ads

Uwoya, Kibonge Sexy na Vita Ya Mapenzi Kisa Patrick

STAA wa filamu Bongo, Irene Uwoya na Mwanamitindo Bhoke Wambura ‘Kibonge Sexy’ wameingia katika vita ya penzi baada ya Uwoya kudaiwa kuwa anamtumia ujumbe mbaya mpenzi wa Kibonge Sex aliyetajwa kwa jina moja la Patrick, ujumbe huo ukimponda Kibonge kuwa si msichana mzuri.
Staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya.
Chanzo makini ambacho ni rafiki wa Kibonge kilichoomba hifadhi ya jina lake kilifunguka kuwa, kisa cha wadada hao kuingia vitani ni kutokana na Uwoya kuwahi ku-date na mwanaume huyo ambaye baada ya kuachana, alimnasa Kibonge Sexy na sasa wana mpango wa kuoana.
KISIKIE CHANZO
“Hivi mnajua kuwa Uwoya na Kibonge hawaelewani kabisa kisa ni penzi la Patrick? Huyu kijana aliwahi kutoka na Uwoya, wakaachana na sasa yupo na Kibonge Sexy, lakini sasa unaambiwa Uwoya kutwa- kucha kumtumia ujumbe mwanaume huyo akimwambia kaingia choo cha kike kwa Kibonge,” kilidai chanzo hicho. Kilizidi kudai kuwa, baada ya Patrick kuchoshwa na maneno ya Uwoya, kupitia ukurasa wake wa Instagram alimtemea ‘sumu’ Uwoya akimuonya kuwa asimfuatefuate, amwache na mwanamke anayempenda (akimaanisha Kibonge Sexy).


UJUMBE WENYEWE SASA…
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Patrick wenye jina la Official_PCK alianza kwa kumsifia Kibonge kisha akaandika ujumbe wa kumuonya Uwoya uliosomeka hivi; Irene wewe nimekupaga nafasi ukaichezea, nimekupa kila kitu ila haukujua thamani yangu so why leo uanze kuniletea maneno ya kumkashfu mwenziyo?
K i b o n g e s e x y asikubabaishe mtu, wewe ndiye mother house, Irene kamlee mwanao, mimi tumeshaachana, usiendelee kuniletea maneno.

Kufuatia fukuto hilo, Risasi Jumamosi lilimsaka Kibonge Sexy ili kupata ukweli wa jambo hilo, naye alifunguka kama ifuatavyo; “Kiukweli Uwoya anajaribu kunichafua kwa mume wangu lakini aache kusumbuka kwani upendo uliopo kati yetu sisi wenyewe ndiyo wenye uwezo wa kuuvunja siyo yeye. “Mimi sikuwahi kugombana naye kwa sababu sikumkuta kwenye uhusiano lakini nashangaa ananifuatilia, namsihi aniache kabisa na amsahau Patrick.”

UWOYA NAYE ASAKWA
Baada ya kuzungumza na Kibonge Sexy, Uwoya naye alivutiwa waya na kusomewa mashtaka yote ambapo badala ya kukasirika, alicheka sana kisha akafunguka kwa kifupi kuwa, eti hamjui Patrick. Waandishi hawakuishia hapo walimtumia ujumbe alioandika Patrick mtandaoni akimpa za chembe, pia alicheka sana na kusisitiza kuwa hamjui.

CHANZO: RISASI JUMAMOSI

No comments