Header Ads

Viongozi Wamiminika Nyumbani Kwa Marehemu Ndesamburo Kutoa Pole Kwa Familia

 

Maandalizi ya mazishi ya marehemu Dkt, Philemon Ndesamburo yakiendelea nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Kwaya ikihudumu kwa nyimbo kwa ajili ya kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akitoa mkono wa pole kwa mjane wa marehemu Ndesamburo, Ndehorio Ndesamburo, alipotembelea nyumbani kwa marehemu kuifariji familia. 
Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe,  akitoa mkono wa pole kwa mjane Ndehorio Ndesamburo nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
...Akitoa mkono wa pole kwa Filomena Ndesamburo, mtoto wa  Ndesamburo nyumbani kwao.
Waziri wa Malisili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe akitoa pole kwa mjane wa marehemu Ndesamburo.
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Idd Juma,  akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
Mkurugenzi wa Halmashauri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Mrema,  akitia saini katika kitabu cha waombolezaji.
Baadhi ya madiwani wakitia saini katika kitabu cha waombolezaji .
Baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa familia ya marehemu Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mstaafu, Saidi Meck Sadiki  (kushoto) akisalimiana na Freeman Mbowe walipokutana nyumbani kwa marehemu  Ndesamburo.
...Akitoa mkono wa pole kwa watoto wa marehemu Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa tatu kulia) akisalimiana na mume wa Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya, Dkt Fidelis Owenya alipofika nyumbani wa marehemu Ndesamburo kutoa salamu za pole.
...Akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini walipokutana nyumbani kwa Ndesamburo.
Mjane wa marehemu Ndeamburo, Bi Ndehorio Ndesamburo (kulia ) akiwa mwenye huzuni.
Baadhi ya waombolezaji .
Mbowe akisalimiana na Askofu wa KKKT Dkt Martin Shoo alipofika nyumbani kwa marehemu  Ndesamburo .
 
Baadhi ya watoto wa marehemu Ndesamburo wakiwa nyumbani kwao.
 
(Picha Na Dixon Busagaga -Kanda ya Kaskazini.)

No comments