Header Ads

Wakazi Wa Pwani Waifurahia Huduma Ya Ukarimu Ya Vodacom


Wakazi wa kanda ya Pwani wameipokea kwa furaha kubwa huduma mpya ya Ukarimu inayotolewa na Vodacom Tanzania wakati huu wa msimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani inayolenga kutoa ushirika na utoaji.
Ukarimu huu wa Vodacom unakwenda samba na kuwapatia wateja kifurushi kinachowawezesha kupata Qaswida, Mawaidha, Hadith, Facebook yenye picha na kuzungumza usiku wanaposubiri daku BURE kabisa.
Ili mteja aweze kunufaika na bando hili la Ukarimu anatakiwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda wa  saa 24 na linalodumu kwa siku saba. Kwa kiasi cha shilingi 1000, mteja atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 10 kwenda mitandao yote, ujumbe mfupi wa maandishi wa maandhishi  bila kikomo, simu kupitia mtandao pamoja na ujumbe wa didi bure.
Kwa mteja atakayenunua bando la shilingi 3000 atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 30 kwenda mitandao mingine, ujumbe mfupi wa maandishi bila kikomo, simu za bure usiku Vodacom kwenda  pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi wa dini bure kwa siku saba.
Siku ya leo Vodacom wanaendelea na futurisha katika maeneo yafuatayo Tangax
•    Nyako
•    Mtindiro Kwabeda
•    Korogwe mjini
Mtwara
•    Newala
Lindi
•    Kilwa somanga
•    Kilwa chumo
•    Ruangwa namungo

No comments