Header Ads

WAKONGWE WA SOKA WAANDAMANA KUMSINDIKIZA ALLY MAYAY KUCHUKUA FOMU YA URAIS TFF


Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayai amechukua fomu ya kuwania nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Jumatatu.

Mayai ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka kwenye vyombo mbalimbali vya habari, aliwasili kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam akisindikizwa na wachezaji wengi wa zamani walioonyesha kumuunga mkono.

Wakongwe hao wa soka waliokuwa na wadau mbalimbali walikuwa na mabango yaliyoandikwa ‘Turudishieni Mpira Wetu’ walikuwa gumzo uwanjani hapo kutokana na watu wengi kuwatazama wao wakati wakiingia na hata mara baada ya mgombea wao kuchukua fomu.
Wakati Mayai anachukua fomu, mshambulizi matata wa zamani wa Simba, Mtemi Ramadhani ‘Mangi’ naye alichukua katika nafasi ya Makamu Rais wa TFF ambaye pia alikuwa pamoja na wakongwe hao wa soka.                       

No comments