Header Ads

Wanawake 4,000 Wajifunza Kuwa Maninja Iran, Kupitia Mbinu za Ninjutsu

Miongoni mwa wanawake 4,000 wanaochukua mafunzo ya uninja jangwani nchini Iran.
WANAWAKE nchini Iran hivi sasa wanajifunza mbinu za wapiganaji wa Ninja kupitia mbinu za Ninjutsu katika klabu ya mafunzo hayo iliyofunguliwa mwaka 1989 iliyopo Jughin, kilomita zipatazo 52 kutoka jiji la Tehran.
Mafunzo hayo yanayofanyika jangwani,  yamelenga kuwafanya wanawake hao kuwa ‘kunoichi’, yaani maninja wa kike.  Katika mafunzo yao wanawake hao wanafanya mazoezi ya kupanda na kuruka kutoka katika kuta mbalimbali, kujificha katika milima na kuweza ‘kukata’ shingo ya adui bila kelele yoyote.
Wanawake wakichukua mafunzo ya uninja katika ngome ya Jughin iliyofunguliwa mwaka 1989 ambako maelfu ya wanawake wanachukua mafunzo.
Mateka ni moja ya mafunzo ya kininja ‘kumsawazisha’ adui.
Ili kuwa ‘kunoichi’ yaani ninja wa kike, inabidi kufanya mafunzo ya nguvu na uvumilivu kama inavyoonekana pichani.
Miongoni mwa mafunzo hayo ni kutumia minyororo dhidi ya adui.
“Wapiganaji” hao wanajifunza kupanda na kuruka kutoka katika milima.
Silaha za hatari ni moja ya mafunzo ya maninja wa kike.
Sensei Akbar Faraji alikuwa mwanamke wa kwanza kuanzisha ninjutsu nchini Iran alipoanzisha klabu hicho miaka 22 iliyopita, leo hii ikiwa na wanachama 24,000.

(HABARI NA MTANDAO/GPL)

No comments