Header Ads

Warriors Yawachapa Cleveland 118 kwa 113 NBA, Usiku wa Kuamkia Leo (Game 3)


ZIKIWA zimebaki sekunde 45.3 kabla ya mchezo kumalizika katika ligi ya mpira wa kikapu (basketball) nchini Marekani, Kevin Durant wa State Warriors aliipatia ushindi timu yake wa magoli matatu ambayo yaliipiga chini Cleveland katika mchezo uliochezwa asubuhi ya kuamkia leo.
Pointi 31 alizotumbukiza golini Kevin ziliwafanya Warriors kufikikisha pointi hizo na hivyo kuongoza ka pointi 3 kwa 0 katika fainali za NBA.
Wakati mchezo ukiendelea, Warriors walikuwa nyuma wakati wa dakika sita za mwisho kabla ya Durant kuchomeka magoli hayo ambayo  yaliwapa ushindi katika mapambano huo wa mwisho.
Ushindi huo umewafanya Warriors kuwa mbele ya timu zote katika msimu wa ligi hiyo.

Stephen Curry (kushoto) na Kevin Durant wakipongezana.
Durant, aliyefunga pointi 31ndiye aliyeipa ushindi timu yake kabla ya sekunde 45 kubakia kufikia mwisho wa mchezo.
Wachezaji wa Cavs (Cleveland) wakiwa wamesononeka baada ya mpambano wao na Warriors.
LeBron James (kushoto) aliyetupia pointi 39 dhidi ya Warriors akiwa amesononeka.
 

 

No comments