Header Ads

Wateja Wa Vodacom Waletewa Bando La Red


Wateja wa Vodacom Tanzania kuanzia sasa watakuwa na furaha zaidi kwa keletewa huduma mpya ya RED. Huduma hii ni mpango unaojumuishwa vifurushi na kulipa kadri utumiavyo. Vifurushi hivi vina dakika nyingi, MB za intaneti nyingi, SMS nyingi na pia dakika za kupiga simu nje ya nchi. Wakati mteja akinunua kifurushi cha RED, anaweza kuchagua huduma ya kifurushi cha kujirudia (kujinunua tena) kila kinapoisha muda wake au kununua mara moja tu.
 

Mteja yeyote yole wa Vodacom akinunua bando ya RED, atapata nafasi na kipaumbele ya kuhudumiwa bila kukaa kwenye foleni wakati akitembelea duka lolote la kampuni hiyo, ambayo yatakuwa na madawati maalum ya RED yatakayokuwa yametengwa kwa ajili yao. Huu ni mpango unaojumuisha vifurushi na kulipa kadri mteja atumiavyo. Vifurushi hivi vina dakika nyingi, MB za intaneti nyingi, SMS nyingi na pia dakika za kupiga simu nje ya nchi. Wakati mteja ananunua anaweza kifurushi cha RED, anaweza kuchagua huduma ya kifurushi cha kujirudia (kujinunua tena) kila kinapoisha muda wake au kununua mara moja tu.

Bando hii ya RED inapatikana kwa kununua kupitia USSD na itadumu kwa muda wa siku 30 kuanzia siku ambayo mteja ameinunua vile vile itakuwa na kipengele cha kujirudia ili kuongeza ufanisi na tunaelewa umuhimu wa kupata taarifa mbalimbali kwa wateja wetu. Wateja wa RED watapata taarifa bure baada ya kumaliza kuongea na simu kuashiria mwisho wa mazungumzo, taarifa ya simu ambazo haujapokea pamoja na matumizi ya data. Tembelea hapa https://goo.gl/j9dU5r kufahamu zaidi kuhusiana na bando hili na tazama video hii ya uzinduzi.

 
Ili mteja ajiunge na kunufaika na kifurushi hiki anatakiwa kupiga *149*01# na Chagua RED na ataona vifurushi vyote vya RED. Ukishajiunga na RED utaweza kufurahia yafuatayo:-
  • Huduma ya SOKONI App BURE
  • Taarifa fupi ya M-Pesa BURE pale atakapoihitaji
  • Huduma ya kipekee pindi atakapowasiliana na huduma kwa wateja.
  • Huduma ya kipekee, pindi atembeleapo maduka ya Vodacom

No comments