Header Ads

Wazazi wa Lulu sasa one Love, Wapatana

MAMA wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael `Lulu’ Lucrecia Karugila anadaiwa kuelewana na mzazi mwenzake ambaye ni baba wa msanii huyo waliyetengana kwa kipindi kirefu. 
 
Kwa mujibu wa chanzo kilichopo karibu na familia hiyo, baba huyo alitofautiana na mama Lulu kwa kipindi kirefu na kwa sasa ameamua kurudisha makazi rasmi anapoishi Lulu na mama yake (Tegeta jijini Dar) jambo linaloashiria kuna maelewano mazuri baina ya wazazi hao yanaendelea.

 Baada ya kuinyaka ishu hiyo, Star Mix lilimvutia waya mama Lulu ambaye alikuwa na haya ya kusema; “Kwani mzazi akiondoka nyumbani akarudi kwake kuna tatizo gani? Baba Lulu ni kama alisafiri sasa ameamua kurudi nyumbani kwake.

No comments