Header Ads

Wema Ajipanga Kutii Wito wa Shehe Mkuu Kufika Ofisini Kwake

Shehe Mkuu wa Dar, Alhad Mussa Salum.
QUEN wa wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu anajipanga kutii wito wa Shehe Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wa kumtaka kufika ofisini kwake kwa ajili ya kisomo maalum ili kumuepusha na mabalaa ambayo yamekuwa yakimuandama.

Siku chache zilizopita Shehe Mkuu wa Dar alimtaka Wema na mama yake, Mariam Sepetu kufika ofisini kwake, Mtaa wa Lumumba jijini Dar ili awafanyie kisomo hicho kufuatia kuandamwa na mabalaa ikiwemo ishu ya mwanadada huyo kutajwa kwenye orodha ya watumiaji wa madawa ya kulevya miezi kadhaa iliyopita ambapo alitakiwa kufika Sentro kwa ajili ya mahojiano na baadaye kupelekwa kwa mkemia Mkuu wa Serikali kupima iwapo anatumia madawa.

Kufuatia sakata hilo Wema na wenzake aliokamatwa nao alifunguliwa kesi kwa tuhuma za kutumia Madawa ya Kulevya.ambayo mpaka sasa bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wema Sepetu

Mbali na madawa ya kulevya, pia kulikuwa na balaa lingine la skendo ya kusambaa kwa sauti iliyodaiwa alikuwa akizungumza mambo ya mapenzi na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

Baada ya kuona kimya tangu shehe huyo alipowaita huku ikidaiwa kuwa hawakutii, Amani lilimtafuta Wema na kumuuliza kulikoni kutotii wito wa kiongozi huyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Nilikuwa na mambo mengi sana ila najipanga, nitaenda kwa sababu hakuna mtu ambaye anaweza kukataa kitu kizuri hasa kutoka kwa shehe, tena shehe mkuu.”

CHANZO: AMANI - GPL

No comments