Header Ads

Wema, Lulu wadaiwa kutumia Makalio Feki, Jipu Pwaaa!

Skendo ya kudaiwa kuwa na kalio feki kwa staa wa filamu Bongo, Wema Abraham Sepetu siyo ngeni kwake na hata kwa mashabiki wake lakini hivi karibuni imeibuka tena baada ya mwanadada huyo kutinga studio na kupiga picha mpya zilizoibua mjadala mkubwa wa shepu yake.

Iko hivi
Baada ya Wema kukihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenda Chadema, aliamua kubadili mfumo wake wa maisha kiasi kwamba hakuwa mtu wa kujichanganya kwenye maeneo ya starehe wala kupiga picha zilizoonesha shepu yake na kuzitupia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kama alivyokuwa akifanya huko nyuma.


Kwa kipindi kirefu, Wema amekuwa akionekana akiwa amevaa madira na mabaibui, mazingira yaliyowafanya mashabiki wake waamini amechoka kujadiliwa kila siku kutokana na umbile lake.

Ashtua mtandaoni
Wakati watu wakifikiria hivyo, staa huyo juzikati alishitua mtandaoni baada ya kutupia picha mpya akiwa amevaa gauni refu lililouonesha sawia ‘msambwanda’ wake na hapo ndipo ule mjadala wa kwamba anajaladia ulipolipuka upyaa.


“Mhh! Mbona hili kalio siyo lile nililolizoea kwa Wema, jamani hili litakuwa la Mchina, hata kama mwenyewe anakataa lakini haliwezi kuwa orijino hili,” alikomenti mmoja wa wafuasi wake.
Mwingine akadakia: “Mbona picha inajionesha? Halafu hili kalio mbona linabadilikabadilika? Kuna kitu anakifanya kwenye hii shepu yake. Ni kweli amefungashia lakini nahisi analiongezea, kama siyo kwa kuvaa zile taiti zao za makalio feki basi anatumia dawa za Kichina huyu.”

Huyu anamtetea
“Nyie mnaosema hivyo mtakuwa hamumjui Wema. Wema kajaaliwa bana, mtoto shepushepu wala hakuna cha Mchina hapo, nishawahi kuona picha zake akiwa swiming pool, mbona nilidata... yaani lile zigo ni orijino,” alisema mchangiaji mwingine aliyeonesha kumjua vizuri staa huyo.

Wema atikisa tena
Wakati mjadala ukiwa ‘hot’ kuhusiana na muonekano huo mpya wa Wema, staa huyo akaamua kutupia picha nyingine akiwa amevaa gauni lenye rangi ya light blue ikilionesha lile zigo lake likiwa kubwa zaidi, hapo ndipo mapovu yalipozidi kuwatoka watu.
Wengi walionekana kutoamini kwamba ni umbo lake halisi na wengine kwenda mbele zaidi kwa kusema, ni kweli mdada huyo amejaaliwa shepu bomba lakini kwa picha hizi mpya kuna kitu amekifanya.
“Unajua mimi nimefuatilia sana huu muonekano mpya wa Wema kwenye hizi picha mbili alizopiga kwa nyakati tofauti, nikawa nataka kujiridhisha kitaalam, nikachukua rula na kupima urefu wa ule msambwanda wake, kwenye ile picha aliyovaa gauni jeusi inaonekana lina sentimita 6 lakini kwenye ile aliyovaa gauni la light blue kalio lina sentimita 9, nimechokaaa...,” alisema kijana mmoja mfuatiliaji wa habari za mastaa aliyejitambulisha kwa jina la Samson.

Wema atoa povu
Alipoulizwa na paparazi wetu kuhusiana na skendo hiyo ya kujaladia kalio lake, Wema alitoa povu akisema: “Nawashangaa sana watu wanaolijadili umbo langu kila kukicha, hawajui mimi nina umbo siyo la kawaida na kwetu tuko hivyo! Wamuangalie mama yangu watapata jibu lakini watu walivyokuwa siyo waelewa utasikia nimetengeneza shepu, kwa sababu zipi nifanye hivyo?
“Niseme tu kwamba nimechoka kuambiwa hili ni kalio feki, I swear (naapa) hili ni orijino na namshukuru Mungu kwa kuniumba hivi kwani kila nguo ninayovaa napendeza, navutia.”

Lulu naye
Naye msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ juzikati aliwashtua wengi baada ya kuonekana akiwa amepuputika kalio, huku wengi wakidai eti picha ambazo anaonekana ana ‘kijungu’ huwa anajaladia.
Lulu alinaswa na paparazi wetu kwenye ‘iventi’ iliyopewa jina la Eid Comedy Gala iliyofanyika siku ya Sikukuu ya Idd kwenye Ukumbi wa King Solomon, uliopo Upanga jijini Dar ambapo alikuwa amevalia kigauni kifupi cha rangi ya damu ya mzee huku akionekana hana kile kijungu tulichozoea kukiona.
Mmoja wa watu waliokuwa ukumbini hapo alisikika akisema: “Haah! Mbona leo Lulu hana lile kalio tulilozoea kuliona? Au ndo’ tuseme na yeye huwa anajaladia kama wanavyofanya mastaa wengine?”
Licha ya minong’ono hiyo, gazeti hili lilifuatilia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuangalia muonekano wake ambapo ilibainika kuwa, kijungu chake kuna picha nyingine kinaonekana kikubwa na nyingine kinaonekana flati, mazingira yaliyoashiria kuwa, figa yake inategemea na nguo  aliyovaa siku husika.

Mwenyewe anasemaje?
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Lulu kuzungumzia madai ya yeye kuwa mmoja wa mastaa wa kike wanaojaladia makalio lakini simu yake haikuweza kupatikana mara moja.

Mastaa wengi wanajaladia
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu umebaini kuwa, mastaa wengi wa kike wakiwa kwenye mitoko yao wanavaa taiti ambazo zinaongeza ukubwa wa makalio yao (angalia picha za ukurasa wa mbele) huku wengine wakidaiwa kutumia dawa za Kichina.

No comments