Header Ads

Yusuf Manji Adaiwa Kuwaongezea Mikataba Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima

BAADA ya kuonekana kuendelea kudorora kwenye mbio za usajili ndani ya Klabu ya Yanga, aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji, anadaiwa kuingilia zoezi la usajili kwa kuwaongezea mikataba baadhi ya mastaa wa klabu hiyo, Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima. 
 
Takribani mwezi mmoja sasa umepita tangu Manji apeleke barua ya kujiuzulu katika nafasi ya uenyekiti wa klabu hiyo, baada ya kudumu kwa miaka mitano mambo yameonekana kwenda taratibu. Licha ya kujiuzulu, baadhi ya wanachama walipinga jambo hilo kwa madai kwamba bado wanahitaji aendelee kuiongoza klabu hiyo. 

Chanzo cha ndani ya klabu hiyo kimesema kwamba, baada ya zoezi la kusajili kuonekana kuwa gumu kwa madai ya kuwa na ukata wa kifedha, wajumbe wa matawi na Kamati ya Utendaji kwa kushirikiana na uongozi uliopo madarakani umemuomba Manji asaidie kufanya usajili. “Manji amekubali kutusaidia kusajili hasa kwa kuwaongezea mikataba wale wachezaji wote waliosajiliwa chini yake hasa wale ambao wanahitajika na mwalimu baada ya kuombwa na baadhi ya wanachama. 

“Ninachoweza kukueleza kwa ufupi tu ni kuwa Manji kawaambia kuwa atawaongezea mikataba wachezaji wote ambao walionekana kushindwa kukaa nao chini kwa kuhofia kutoweza gharama za usajili wao. 

“Hadi hapa ninapokuambia tayari Ngoma, Kamusoko, Niyonzima, Tambwe na wengine wote ambao walienda mapumziko wametaarifiwa warudi Dar ili waje kukaa chini na kuongeza mikataba yao ambayo imeshafikia mwisho. “Kuna wachezaji wa ndani kama Deogratius Munishi ‘Dida’ na Haji Mwinyi tayari wameshaongeza mikataba yao, hivyo wanasubiriwa wale ambao wapo makwao.

No comments