Header Ads

AY Amvalisha Pete Mchumba Wake, Ndoa Yanukia

Rapper nguli asiyechuja tangu kitambo hicho kutoka Bongo Fleva, Ambwene Allen Yessayah maarufu kama A.Y ama ‘Mzee wa Ankara’, ‘Mzee wa Commercial’ amedhihirisha kuwa kwa sasa yuko tayari kuachana na ukapela baada ya kumvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu, Remy.
Tukio hilo lilifanyika jana Alhamisi ambapo A.Y alimvalisha pete mrembo huyo ambaye ni raia wa Rwanda na amekuwa naye katika mahusiano tangu mwaka 2008Hakika ni furaha.

Kwa mara ya kwanza AY alimtambulisha mpenzi wake huyo Desemba mwaka jana wakati wa siku ya kuzaliwa ‘birthday’ ya mrembo huyo.Pete imo kidoleni.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu wa karibu na wawili hao. Kwa kitendo hicho tunatarajia kuiona ndoa ya A.Y na mpenzi wake huyo siku chache zijazo akiwafuata mastaa wengine kama MwanaFA, R.O.M.A, Prof, Jay ambao wamefunga ndoa na wana-enjoy maisha ya familia.
Picha na Mx Carter

No comments