Header Ads

BAADA YA SEKESEKE, SASA KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF KUKUTANA KESHO


LeoJumamosi ndiyo siku ambayo Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya mwenyekiti wake, Wakili Revocatus Kuuli,
inatarajiwa kukutana kwa ajili ya kupanga mikakati yao ikiwemo siku ya kuendelea kwa mchakato wa Uchaguzi wa TFF uliositishwa.

Ikumbukwe kuwa katika siku za hivi karibuni, Kuuli alitangaza kusitisha mchakato wa uchaguzi huo baada ya wajumbe wa kamati hiyo kudaiwa kuvunja kanuni kutokana na kutaka kupitisha baadhi ya majina ya wagombea bila ya kufanyiwa usaili.

Baada ya kusitishwa kwa mchakato huo, Jumanne ya wiki hii, Kamati ya Utendaji ya TFF, ilikutana kujadili mustakabali wa Uchaguzi wa TFF, ambapo mwisho wa siku wakaiunda upya kamati hiyo.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amekiri juu ya kamati hiyo kukutana ili kuendeleza mchakato huo wa uchaguzi ambao ulianza kuvurugika baada ya baadhi ya wagombea kukosekana kwenye usaili akiwemo rais wa sasa wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi ambaye yupo mahabusu.

No comments