Header Ads

Ben Pol Kwenye Penzi Zito na Ebitoke Usiku wa Saida Karoli (VIDEO)


MKALI wa ngoma za R&B/soul  anayetamba na wimbo wake mpya wa Tatu aliomshirikisha Darassa, Ben Pol amejikuta akinasa kwenye penzi zito na msanii mwenzake wa Komedi, Anastazia Exavery ‘Ebitoke’ (19) ambaye hivi karibuni amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa umahiri wake wa kuifanyia kweli tasnia hiyo ya vichekesho.

Wawili hao walinaswa usiku wa kuamkia leo wakiwa wameketi pamoja wakati wa Shoo ya Miaka 15 ya Saida Karoli iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Escape One, huku kukiwa na kila ishara kwamba kwa sasa wapo couple.

Baada ya Global TV Online kumdaka Ben Pol alikuwa na haya ya kuzungumza kuhusu penzi lao.

“Nimempigia simu akiwa nyumbani kwake, tukapanga tutoke twende kwenye shoo na tukakubaliana tuvaeeje. Malengo kati yangu na Ebitoke ni siri yetu, vitu vingine ni binafsi siwezi kuvizungumza hapa lakini sisi ndo tunajua.
“Kikubwa nachoweza kusema ni kwamba Ebitoke ni mwanamke mzuri kama nilivyosema siku ya kwanza nikifanya interview na Global TV Online. Kwa hiyo nitaendelea kusema nilichokimaanisha sikuteleza. Ebitoke ni mwanamke mzuri, anajituma, ni jasiri  na anapenda mafanikio,” alisema Ben Pol.

Ebitoke alikuwa na haya ya kunena;
“Mimi niliwambia watu wajue kwamba hii siyo kiki, tutawa-proove kwamba ni kweli, waendelee kusubiri.”
Wawili hao wakazama vifuani na kukumbatiana.

No comments