Header Ads

Chelsea Kumpeleka Matic Inter Milan

 

Kiungo Nemanja Matic wa Chelsea
KLABU ya Inter Milan inatarajiwa kutuma ofa ya kumsajili kiungo Nemanja Matic wa Chelsea baada ya klabu hiyo kukataa kumuuza mchezaji huyo kwenda Manchester United.
Uhusiano wa United na Chelsea haupo sawa baada ya United kumsajili Romelu Lukaku wa Everton ambaye alikuwa akiwaniwa kwa ukaribu na Chelsea.
Taarifa kutoka Italia zinaeleza kuwa, Chelsea ipo tayari kumpeleka Matic Italia kuliko aende United hasa endapo itafanikiwa kumsajili  Tiemoue  Bakayoko  wa Monaco ambaye anawaniwa na United

No comments