Header Ads

Feza Kessy: Kuna media hata interview nabaniwa

Msanii wa Bongo Flava na Mtangazaji wa Choice FM, Feza Kessy amesema kutokana na kazi yake ya utangazaji kuna baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa havimpi support.

Muimbaji huyo amedai kabla ya kuingia katka utangazaji mambo yalikuwa tofauti na sasa, na kuviomba vyombo hivyo vya habari vitenganishe kazi yake na muziki.
“Kwa mfano mimi kuwa CMG unakuta media zinaogopa, sijui wanavyowaza wao lakini support inakuwa inapungua. Ningependa ile support ya muziki iendelee kama walivyokuwa wanafanya mwanzo, sasa hivi wamepunguza kasi kuna sehemu hata interview nabaniwa,” ameiambia XXL ya Clouds FM na kuongeza.
“Kuna media nyingine wanacheza lakini kuna specific media ambazo hata interview nilishindwa kupata. Siwezi kutaja kwa sasa hivi ila wajue this is business, ni kazi yangu as an individual wasini-judge kikampuni,” amesisitiza.
Feza Kessy kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Kaa Kijanja’ ambao amemshirikisha rapper kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili.

No comments