Header Ads

Halima Mdee(Mb, CHADEMA) akamatwa na Polisi. Apelekwa Oysterbay...

Hii ni SMS yake baada ya kukamatwa!
"Wamekuja polisi kunichukua home! As we speak naelekea kituo cha polisi, probably Oysterbay Au Central. Wasaidizi wangu watakuwa na taarifa zaidi za ninakoelekea!
1916295_1208970312454206_538259505458926396_n.jpg
Halima Mdee!

Katibu wa CHADEMA jijini Dar, Henry Kilewo amesema Mbunge huyo wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA), ni kweli amekamatwa na Polisi na kupelekwa kituoni Oysterbay.

Mapema leo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi alitoa agizo la kukamatwa kwa Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima James Mdee mara moja kwa kosa la kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli.

No comments