Header Ads

HII NDIYO KAULI YA IBRAHIM AJIBU BAADA YA KUTUA YANGA


Ibrahim Ajibu amefurahi kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na amedhamiria kuweka rekodi yake kwenye klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo mpya wa Yanga, amewataka mashabiki wa timu hiyo kutarajia mambo makubwa kutoka kwake kwani amedhamiria kuifikisha mbali timu hiyo msimu ujao.

Akizungumza baada ya kumalizana na Yanga kitokea Simba, Ajibu anasema: "Ukweli nimefurahi sana kuona mimi ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga timu bora Tanzania, kwa kulitambua hilo nimejipanga kutoa mchango wangu ili kuchangia mafanikio ambayo yatazidi kuifikisha mbali zaidi ya hapo ilipo,"

"Nawashukuru mashabiki wa Yanga kwa kunipokea vizuri na mimi nawaahidi mambo mazuri, ambayo yatawafanya msijutie ujio wangu hapa na hakuna kingine zaidi ya kuwapa makombe mengine," amesema Ajibu.

Mshambuliaji huyo pia amewashukuru mashabiki wa timu yake ya zamani ya Simba kwa sapoti kubwa waliyompa wakati akiitumikia timu yao na kuwaambia siku zote atawakumbuka kwasababu wao ndiyo waliosababisha afikie hapo alipo.

Amesema kwa sasa yeye ni mchezaji wa Yanga na akili yake kwa sasa inawaza kuisaidia timu yake iweze kufikia mafanikio yaye ambayo timu itakuwa imejiwekea kwa mismu ujao na mingine.

Ajibu amesema kitu ambacho amepania kukifanya akiwa na Yanga ni kubeba ubingwa wa Ligi ya Vodacom ili naye awe sehemu ya mafanikio na rekodi za timu hiyo kubeba taji hilo mara nne mfululizo.

CHANZO: GOAL

No comments