Header Ads

Jina Jayden K Smith Latumika Kusambaza Meseji Feki ya Udukuzi

WATUMAJI wa mtandao wa kijamii wa Facebook wamekuwa wakibabaishwa na meseji yenye ujumbe feki inayowaonya wasipokee maombi ya urafiki kutoka kwenye akaunti inayoitwa Jayden K Smith. Meseji hiyo inayopitia Facebook Messenger, inaonya kwamba akaunti hiyo ni ya mdukuaji wa mitandao “aliyeunganisha mfumo huo na akaunti yako ya Facebook”. Wanaotilia maanani meseji hiyo, wanaisambaza kwa watu wengine, lakini kutokana na meseji nyingi za Facebook, meseji hiyo ni ya uongo. Hakuna ushahidi unaoonyesha akaunti yenye jina la Jayden K Smith kusambaa kwa watumiaji, na kama ipo, haiwezi kudukua akaunti yoyote kwa kukubaliwa kuwa rafiki na mtumiaji. Isitoshe, kanuni za Facebook zinakataza watu wenye akaunti kuwa na marafiki wengi wasiojulikana, jambo ambalo linaweza kuwa rahisi kukabiliana na jambo hilo.  
Ujumbe huo umekuwa ukisomeka kwamba: "Tafadhali waambie washirika wako wote wa katika orodha yako ya Messenger, waambie wasikubali maombi ya urafiki na Jayden K Smith. Huyo ni mdukuaji na mfumo wake wa udukuzi ameuunganisha kwenye akaunti yako ya Facebook. Iwapo mmoja wa watu unaowasiliana nao atamkubali, utajikuta na wewe unafanyiwa udukuzi, hivyo hakikisha marafiki zako wote wanafahamu jambo hili. Asante. Ujumbe umeletewa kama ulivyopokelewa." Meseji hiyo ni moja ya zile zinazotishia wenye akaunti kwenye Facebook kuhusu mambo mbalimbali.

No comments