Header Ads

Kagera: Wajanja wamemdanganya Mbaraka
 UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa, kuna wa¬janja wachache wamejitoke¬za kumdanganya mshambuliaji wao Mbaraka Yusuph kwa lengo la kupiga fedha na kudai kuwa watakutana TFF na Azam kubaini nani mwenye haki.
Mbaraka ambaye amesaini Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili, inase¬mekana ana mikataba ya aina mbili, ule wa miaka miwili na wa miaka mi¬tatu Kagera Sugar, jambo ambalo lina¬muweka njia panda mchezaji huyo ka¬tika msimu ujao wa ligi kuu. 


Akizungumza na Championi Ju¬matatu, Meneja wa Kagera Sugar, Mo¬hamed Hussein ameeleza kuwa kwa upande wao hawana neno, wanas¬ubiria chombo chenye mamlaka TFF kiweze kutoa maamuzi juu ya mchezaji huyo ambaye ameingia chaka kutoka¬na na wajanja wachache kumdanganya kwa ajili ya kupiga pesa. 


“Jina la Mbaraka litajitokeza katika timu mbili msimu ujao lakini kwa up¬ande wetu sisi hatuna la kusema, tu-nasubiria uchaguzi umalizike ili wa¬husika watoe maamuzi juu ya mchezaji huyo.
“Mchezaji ameshindwa kujitambua baada ya kuona amefanya vizuri na kusahau nyuma na kupata wajanja wachache waliomdanganya na kua¬mua kumpeleka Azam bila ya kuangalia mkataba wake wa huku, lakini mwisho wa siku TFF ndio watakaoamua. 


“Kuna wakati Azam walikuja juu ka¬tika mtandao wao lakini wanapaswa kutambua kuwa kesi yetu sisi ipo na Mbaraka na si Kagera dhidi ya Azam kama wanavyoeleza kuwa wameona mkataba wake, hilo jambo halituhusu sisi, tunachojua ni mchezaji wetu halali. 


“Sisi tulifanya mazungumzo na Sim¬ba na Yanga kwa ajili ya kumuuza huko lakini kabla hatujamalizana nao, kuna wajanja wamemchukua na kumpeleka Azam, ngoja tusubiri,” alisema Moham¬ed.
Championi lilifuatilia TFF kubaini ukweli juu ya jambo hilo, likataarifiwa kuwa mkataba wa Kagera na Mbaraka wa miaka miatatu ndiyo halali na siyo ule wa miaka miwili anaodai mchezaji

No comments