Header Ads

KAULI YA YANGA KUACHANA NA DIDA YAWASHITUA YANGA
Kauli iliyotolewa na Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali kuwa wameachana na kipa wao Deogratius Munish ‘Dida’ imeonyesha kuwashitua mashabiki wengi wa klabu hiyo.

Wengi wamekuwa wakihoji sababu ya Dida kuondoka na wengine wakimtaka kuvuta subira.

Lakini wako mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiutaka uongozi wa Yanga kukaa na kumalizana naye vizuri.

Wengine wameshauri kama amepata timu nje aende lakini si hapa Tanzania.

Pondamali alisema Dida aliwaambia hatasaini mkataba na juhudi za kumbembeleza zimekwama.


Hivyo kipa African Lyon waliyemsajili, Beno Kakolanya waliyenaye na watasajili kipa mwingine chipukizi.

No comments