Header Ads

Kidoa Anamiliki nyumba maeneo ya Chanika, Dar ... siyo wa mchezomchezo

MSANII wa filamu Bongo, Asha Salumu ‘Kidoa` amethibitisha kuwa yeye sasa siyo wa mchezomchezo baada ya kufanikiwa kumiliki nyumba maeneo ya Chanika, jijini Dar es Salaam baada ya kujikita pia kwenye tamthiliya ya Huba, jambo linalomfanya asifikirie mambo ya u video queen kwa sasa.

Akipiga stori na Za Motomoto News, alisema tangu ajikite kwenye ishu hiyo amebadilisha maisha yake kwani sasa ameweza kumhamisha mama yake kutoka nyumba ya kupanga aliyokuwa anaishi maeneo ya Kinondoni Dar.

“Namshukuru Mungu, tamthiliya zinanilipa kwa kweli sikutarajia kwa umri huu mdogo wa miaka 22, ningeweza kumiliki mjengo tena kwa jasho langu, hatimaye nimemnusuru mama yangu na mabalaa ya nyumba za kupanga,” alisema Kidoa.

No comments