Header Ads

Kuagwa kwa marehemu 'Bikira wa Kisukuma' Viwanja vya Leaders, Dar

MWILI wa marehemu Seth Katende 'Bikira wa Kisukuma', aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, kipindi cha Ubaoni, umeagwa katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya kumalizika kwa shughuli hizo, safari ya kuelekea kwenye makazi yake ya milele, kwenye Makaburi ya Kinondoni ilianza ambapo hatimaye maziko yamefanyika mchana wa Juni 12, 2017.
Bikira wa Kisukuma, alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyakazi wenzake ambao hawakutaka kutajwa majina yao kwa vile siyo wasemaji, walisema marehemu alianza kuugua kiasi cha mwezi mmoja uliopita na msiba uko nyumbani kwa baba yake mzazi huko Changanyikeni.

Marehemu ambaye alikuwa akitangaza kipindi cha Ubaoni, kinachorushwa na redio hiyo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa kumi jioni, alikuwa pia ni bloga maarufu katika mitandao ya kijamii

No comments