Header Ads

LUKAKU USAJILI MWINGINE WA KUSHANGAZA BARANI ULAYA

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho.
JULAI 10, mwaka huu, Manchester United chini ya Kocha Jose Mourinho, ilimsajili straika Romelu Lukaku kutoka Everton kwa dau la pauni milioni 75. Usajili wa Lukaku ulikumbana na misukosuko mingi na wengi walidhani straika huyo raia wa Ubelgiji angesajiliwa Chelsea na siyo Man United. Mambo yakawa ndivyo sivyo.
Chelsea ndiyo iliyotajwa muda mrefu kumuwania Lukaku ikiamini straika huyo angekubali kurejea kikosini hapo alipoonekana hana msaada wakati timu yao ikifundishwa na Mourinho. Wengi walidhani uhusiano usio mzuri kati ya Lukaku na Mourinho ungeisaidia Chelsea kumsajili mchezaji huyo.
Hata hivyo, Mourinho aliweka vizuri uhusiano wake na Lukaku kisha akamsajili na kuwaacha Chelsea wakishangaa. Sasa ugomvi upo kati ya Chelsea na Man United na klabu hii ya London imekataa kuiuzia Man United, kiungo wao Nemanja Matic, ishu ni hiyohiyo ya Lukaku. Hapa chini ni baadhi ya sajili zilizotokea katika hali ya kushangaza na nyingine kuzua utata;
Romelu Menama Lukaku alipokuwa katika timu ya Everton.1 JOHN OBI MIKEL
Lyn kwenda Chelsea (2005) Kiungo John Obi Mikel alikuwa na miaka 18 tu mwaka 2005 akichezea Lyn ya Norway, hapo Chelsea na Man United zikamuwania. Mikel akasaini Man United na akafanya mkutano na waandishi wa habari, baadaye Chelsea ikaibuka na kusema imemsajili, Man United walikasirika na kuifi kisha kesi hiyo kwa Chama cha Soka England (FA) lakini hawakuweza kushinda.
2 JOHAN CRUYFF
Ajax kwenda Feyenoord (1983) Gwiji wa soka Johan Cruyff  alifariki Machi 24, mwaka jana lakini alichanganya watu jijini Amsterdam, Uholanzi mwaka 1983 alipohama kutoka Ajax kwenda Feyenoord. Ajax ilitoka kutwaa ubingwa wa Uholanzi na haikuwa imemuongezea mkataba Cruyff  ikidhani ingefanya hivyo muda wowote ule, jamaa akaamua kwenda Feyenoord huku Ajax wakiamini asingeweza kufanya hivyo. Cruyff  aliipa ubingwa mara mbili mfululizo Feyenoord kisha akarejea Ajax kama kocha.
Lukaku akifanya mazoezi na timu ya Man Utd.3 ROBIN VAN PERSIE
Arsenal kwenda Man United (2012) Robin van Persie alikuwa kipenzi na roho ya mashabiki wa Arsenal, lakini ghafl a mwaka 2012 akadai anataka kuondoka klabuni akisema ameshafanya mambo mengi, hakueleweka lakini baadaye Bodi ya Arsenal ikiwa na Kocha Arsene Wenger ilibidi tu wakubaliane naye. Van Persie akatua Man United, mashabiki walikasirishwa na hali hiyo na hawakuamini. Van Persie alizomewa kila alipokutana na mashabiki wa Arsenal.
4 ASHLEY COLE
Arsenal kwenda Chelsea (2006) Beki Ashley Cole alionekana ni kijana wa Arsenal kwani alikulia katika timu hiyo, lakini ghafl a mwaka 2006 baada ya kucheza misimu sita, akataka aongezwe mshahara hadi pauni 60,000 kwa wiki lakini Arsenal ikasema inaweza kumlipa pauni 55,000 kwa wiki, akakataa ndipo Chelsea ilipokubali kumlipa pauni 90,000 kwa wiki, naye akaondoka. Mashabiki wakachukizwa na uhamisho wake wakimuona ni mpenda fedha ambapo walimpachika jina la Cashley.
5 ROBERTO BAGGIO
Fiorentina kwenda Juventus (1990) Mwaka 1990 Roberto Baggio alikuwa staa kwelikweli, waka ti h u o akichezea Fiorentina timu aliyoipenda kutoka moyoni. Ghafl a mwaka huohuo akajiunga na Juventus kwa dau la dola milioni 8 na kuvunja rekodi ya usajili. Mashabiki waliandama mitaani na kufanya vurugu huku wengine wakijeruhiwa. Katika mechi dhidi ya Fiorentina, Baggio aligoma kupiga kona na hapo hapo akatolewa uwanjani na akiwa anaelekea vyumba vya kubadilishia nguo, aliibusu skafu ya Fiorentina na kusema; “Kitu kilicho moyoni mwangu, muda wote mimi ni zambarau.”

6 ALFREDO DI STEFANO
Millonarios kwenda Real Madrid (1953) Ilibaki kidogo yule gwiji wa zamani wa Real Madrid atue Barcelona mwaka 1953 badala ya kwenda Madrid. Di Stefano alijiunga na Millonarios ya Colombia mwaka 1949 akitokea River Plate Argentina. River Plate ikadai bado inammiliki Di Stefano ikaanza kuzungumza na
Barcelona kuhusu usajili wakati Madrid wao wakizungumza na Millonarios. Madrid fasta ikamtangaza Di Stefano kuwa mchezaji wao. Utata huo wa usajili uliingiliwa na Dikteta wa Hispania, Francisco Franco aliyeilazimisha Barcelona imuache Di Stefano aende Madrid ambao ni mji mkuu wa dikteta huyo. Barcelona iliona ni uonevu na hadi leo bifu lipo kati yao na bifu hilo likakomaa zaidi katika El Clasico
7 SOL CAMPBELL T
ottenham kwenda Arsenal (2001) Pale nahodha anaposema kamwe hawezi kujiunga na timu wapinzani wa jadi, kila shabiki ni rahisi kuamini hivyo. Hata hivyo, Sol Campbell aliwasaliti Tottenham Hotspur na kwenda Arsenal mwaka 2001, alichukiwa na  mashabiki lakini hakujali.
8 LUIS FIGO
Barcelona kwenda Real Madrid (2000) Hadi leo Luis Figo anachukiwa na mashabiki wa Barcelona, kwani Julai 24, 2000 alisema a n g e b a k i Barcelona kutetea ubingwa wa La Liga, k e s h o yake tu akasajiliw a na Real Ma- d r i d , balaa l a k e si la ki- toto. Mche- z o mzima al- icheza Rais wa Madrid wakati huo, Florentino Perez akitaka aonekane asiyeshindwa kitu, alimsajili Figo kwa pauni milioni 62, na zilikuwa nyingi mno wakati huo hadi sasa. Mashabiki wa Barcelona walimrushia Figo kichwa cha nguruwe miaka miwili baadaye akicheza dhidi yao.

No comments