Header Ads

Mali za mume wa Zari zapigwa bei, Alichoambulia Zari Mmh!

Aliyewahi kuwa mume wa staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, marehemu Tycoon Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ (kulia) enzi za uhai wake. Kushoto ni Zari.
AMA kweli asiyekuwepo na lake halipo! Habari zilizolifi kia Amani mapema wiki hii zimeeleza kuwa, wakati aliyewahi kuwa mume wa staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ (40), akiwa hajatimiza hata miezi miwili kaburini, tangu alipofariki dunia, tayari mali nyingi alizoziacha zimeanza kupigwa bei mdogomdogo.
Mara baada ya kifo Mei 25, mwaka huu na mazishi ya Ivan yaliyofanyika Mei 30, kijijini kwao huko Nakalilo nchini Uganda, kuliibuka utata mkubwa juu ya umiliki wa utajiri wa kutisha aliouacha mfanyabishara huyo nchini humo na Afrika Kusini.

ZARI AAMBULIA ASILIMIA 50
Lakini mwisho wa vikao lukuki vilivyofanyika nchini humo chini ya familia ya jamaa huyo, Zari ambaye alizaa na Ivan watoto watatu wa kiume kabla ya kutengana naye na kuwa na mwanaume mwingine ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, aliambulia asilimia 50 ya utajiri huo. Habari kutoka kwenye vyanzo vya Uganda zilidai kuwa, sehemu nyingine ya utajiri wa Ivan ilibaki upande wa familia yake hasa mali zilizopo nchini humo ambazo ndizo zinazosemekana kuanza kuwekwa sokoni.
WAANZA NA JUMBA LA KIFAHARI
Ilidaiwa kuwa, wakati kukiwa na madai ya kuanza kuuzwa mali hizo yakiwemo magari yake ya kifahari, hivi karibuni, kampuni maarufu ya kununua na kuuza nyumba (real estate) nchini humo, ilitoa tangazo kwenye mitandao yake ikitangaza kuuza moja ya majumba ya kifahari ya Ivan iliyopo Munyonyo jijini Kampala. Kwa mujibu wa mtandao maarufu wa habari za udaku nchini Uganda, kampuni hiyo ilitangaza kuuza jumba hilo la Ivan ambalo lilikuwa makao makuu ya kundi la vijana matajiri la Rich Gang lilioongozwa na Ivan.

Habari hizo zilieleza kuwa, jumba hilo ndiyo lililokuwa likimpa heshima kubwa Ivan kutokana na ukubwa wake na kusheheni samani za kisasa huku likilinganishwa na majumba ya kifahari ya mastaa wa muziki na michezo duniani ambao husifi ka kwa kumiliki mijengo ya bei mbaya.

LINAUZWA BIL. 3.6
Ilidaiwa kwamba, jumba hilo limewekwa sokoni kwa dau la dola milioni 1.7 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 6.1 za Uganda na ni zaidi ya shilingi bilioni 3.6 za Kibongo. Kwa mujibu wa tangazo hilo, jumba hilo lina vyumba sita vya kulala vinavyojitegemea (selfcontained), sebule kubwa, chumba cha mapumziko, dinning (sehemu ya chakula), gym (sehemu ya mazoezi), baa na makorokoro mengine ya ndani huku nje ikizungukwa na parking (maegesho ya magari), swimming (bwawa la kuogelea) na bustani baab’kubwa.
MAJIBU YA WAUZAJI
Mtandao huo wa udaku uliwasiliana na uongozi wa kampuni hiyo ili kupata ufafanuzi juu ya kuuzwa kwa mjengo huo ambapo majibu yalikuwa hivi: “Unataka kununua au unataka kujua tu? Wewe una shida gani? Kwa nini usiendelee na shughuli zako?” Taarifa nyingine za ndani kutoka kwa Mbongo aliyekuwa rafi ki wa Ivan zilidai kuwa, wakati kukiwa na taarifa za kuuzwa kwa jumba hilo, juzikati mtangazaji maarufu wa runingani nchini humo, Anita Fabiola alionekana akijiachia kwenye bwawa la kuogelea katika nyumba hiyo.
KWA NINI ZINAPIGWA BEI? Rafi ki huyo wa Ivan alisema kuwa, tukio la Anita kujiachia kwenye mjengo huo kuliibua gumzo kuwa huenda alikuwa akifanya matangazo ili kupata mteja wa haraka kwa sababu muda mfupi baadaye alitupia picha hizo kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Snapchat. Jamaa huyo alidai kwamba, ndugu wa Ivan walifi kia hatua hiyo ya kuuza baadhi ya mali ili kulipa madeni na kurejesha mikopo ambayo jamaa huyo anadaiwa na watu mbalimbali wakiwemo marafi ki zake ambao walikuwa wakishirikiana naye kwenye biashara zao.

MALI NYINGINE
Ukiacha magari na jumba hilo la kifahari, Ivan pia ameacha mali nyingine nyingi yakiwemo majumba mengine mawili, moja likiwa Pretoria na lingine Sandton, Afrika Kusini. Mali nyingine ni mashamba makubwa nchini Uganda, vyuo vya unesi, urembo na ulinzi na hoteli ya nyota tano aliyokuwa akimalizia ujenzi wake iliyopo Kampala. Ivan aliyesifi ka kwa kusaidia watu wenye shida alifariki dunia Mei 25, mwaka huu kutokana na shambulio la moyo.

No comments