Header Ads

MAMA KIBA ATEMA CHECHE MADAI YA KIBA KUZAA NA BINTI WA KENYA

Msichana mmoja kutoka Kenya aliyefahamika kwa jina la Nuru Hatim akiwa na mtoto anayedaiwa wa Ali Kiba
SKENDO ‘hot’ inayomhusu staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’ ya kudaiwa kuzaa na msichana mmoja kutoka Kenya aliyefahamika kwa jina la Nuru Hatim kisha kumtimua, imechukua sura mpya baada ya mama wa msanii huyo kuzungumza na gazeti hili na kutema cheche, Ijumaa linakujuza.
[caption id="attachment_144745" align="aligncenter" width="600"]  
Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Ali Kiba’.
KUHUSU BINTI MKENYA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Nuru alitua Bongo akitokea nchini Kenya na kwenda kwenye Kituo cha Polisi cha Msimbazi na pia Ubalozi wa Kenya nchini Tanzania kwa ajili ya kuomba msaada wa kumpata Kiba sambamba na kuomba msaada wa kisheria akidai amezaa na staa huyo kisha kuachwa kwenye mataa.
Staa wa Bongo, Jokate Urban Mwegelo 'Kidoti'.[/caption]TUJIKUMBUSHE KWANZA ALICHOKISEMA NURU
“Mwaka jana nikiwa Mombasa, Kiba ambaye tulikuwa tukijuana na kuwasiliana kwa muda mrefu, alikuja kufanya shoo na ndipo tulipofanya tendo la ndoa.
“Mara kadhaa tulikuwa tukikutana kwa kutumia kinga lakini safari hiyo, hatukutumia na ndipo nikanasa mimba.
“Baada ya kunasa mimba, familia ilinijia juu na kutaka kujua mhusika, nikawaambia ni Kiba ndipo nilipofukuzwa na kwenda kuishi na rafiki zangu. Kiba alikuwa hapatikani mpaka najifungua, ndiyo nikaja Bongo na kwenda nyumbani kwa akina Kiba ambapo mama yake aliniambia hayupo, amesafiri,” alisema msichana huyo aliyekuwa amempakata mtoto anayeonekana kufanana na Kiba.
Baada ya habari hiyo kuwa gumzo kubwa, Kiba alitafutwa kupitia simu yake ya mkononi lakini hakupatikana licha ya juzikati kudaiwa kuongea na redio moja nchini Kenya na kusema kuwa, kitakachofuata baada ya
msichana huyo kumwaga mboga ni kipimo cha DNA.

IJUMAA LAMSAKA MAMA YAKE KIBA
Baada ya hayo yote kujiri, waandishi wetu walifunga safari hadi nyumbani kwa wazazi wa Kiba na kufanikiwa kuzungumza na mama yake kuhusiana na mjukuu wake huyo mpya kutoka Kenya. Mahojiano yalikuwa hivi:
IJUMAA: Mama bila shaka umesikia juu ya huyu dada ambaye amekuja nchini na kusema amezaa na mwanao lakini amemtelekeza. Una lipi la kuongea?

MAMA KIBA: Nimesoma hiyo habari kwenye gazeti leo (Jumanne), wakati natoka kwenye shughuli zangu lakini nilikuwa sijazisikia kabisa.
IJUMAA: Haya, kwa kuwa umezisikia utachukua hatua gani ili kuhakikisha huyo dada na mwanaye wanapata msaada?
MAMA KIBA: Hakuna hatua nitakazochukua, ingekuwa Ali mwenyewe kaniambia kuwa huyo ni mwanaye, ningeweza kufanya lolote. Lakini katika hili siwezi kufanya lolote kwa sababu kwanza sina uhakika kuwa ni mwanaye na ni jambo ambalo halinihusu.
IJUMAA: Halikuhusu kwa sababu hujashirikishwa na mwanao ama halikuhusu kivipi? Hebu fafanua kidogo.
MAMA KIBA: Kwa sababu Ali hajaniambia kitu kama hicho. Unajua masuala haya ya wanawake kuibuka na kusema wamezaa na hawa watoto huwa yanajitokeza mara kadhaa.
Hata kwa Abdu (Abdu Kiba), alishawahi kuja mwanadada sijui anatokea Dubai sijui wapi na kusema amezaa naye lakini haikuwa kweli, ni kama alikuwa ametengenezwa tu ili kufanikisha vitu ambavyo hakuna anayeweza kuvielewa ama kuvielezea vikaeleweka.
IJUMAA: Sawa mama. Lakini Kiba ana watoto kadhaa ambao wamekuwa wakiandikwa na kusemwa kwenye vyombo vya habari, vipi kwa upande wako umewahi kuwasikia ama kuwaona?
MAMA KIBA: Ni mtoto mmoja tu aitwaye Samir ndiye nina taarifa naye sahihi. Huyu mimi ndiye nilimdai baada ya kumuona kwenye Laptop ya Ali wakati ananionyesha picha za shoo aliyoifanya Paris.
Baada ya kumuona moyo ulinilipuka maana mtoto huyo alikuwa anafanana na Ali wakati yupo mdogo. Ikabidi nimdai na nikaletewa.
Watoto wengine nimekuwa nikiwasikia tu, kuna mkubwa ana miaka nane wa kike na mwingine mdogo, lakini sijawa na taarifa nao sawasawa.
IJUMAA: Na kuhusu mama zao na hao watoto pamoja na wapenzi wengine ambao amekuwa akitoka nao, kuna hata mmoja ambaye amewahi kukutambulisha kuwa atamuoa?
MAMA KIBA: Hapana. Kwanza wanangu sijawalea kwenye maadili mabaya kiasi hicho kiasi kwamba wanihalalishie zinaa. Kwa hiyo sijatambulishwa mwanamke yeyote yule.
IJUMAA: Vipi kuhusu Jokate?
MAMA KIBA: Amefanya nini?
IJUMAA: Hujawahi kufahamu kuwa anatoka kimapenzi na mwanao?
MAMA KIBA: Ninachofahamu ni rafiki yake na walikuwa wanashirikiana kwenye kazi, basi!
Baada ya cheche hizo za mama, waandishi wetu pia walitaka kujua mwanadada Jokate Mwegelo aliyewahi kuwa na uhusiano na Kiba hadi kufikia hatua ya kusema atamzalia mtoto, ana lipi la kusema juu ya kuibuka kwa Nuru na kudai amezaa na X-boyfriend wake.
Katika hali ya kushangaza, Jokate alitoa povu kama
inavyoonekana kwenye mahojiano haya hapa chini.
Ijumaa: Kuna madai ya mpenzi wako, Ali Kiba kuzaa na binti kutoka Mombasa, unaliongeleaje hilo?
Jokate: Inanihusu nini sasa mimi?
Ijumaa: Wewe kama uliyekuwa mpenzi wa Ali Kiba.
Jokate: Mwandikeni yeye (Ali Kiba) na huyo mwenye mtoto wake.
Ijumaa: Nilijua povu litatoka lakini ungesema lolote basi jamani.
Jokate: Sitoi povu nakueleza tu. Msinihusishe kwenye vitu vichafuchafu.
Habari hii imeandikwa na Boniphace Ngumije, Ally Katalambula na Imelda Mtema.

CREDIT - GLOBAL PUBLISHERS

No comments