Header Ads

MCHEZAJI WA SIMBA AIBUKIA KWENYE MAZOEZI YA YANGA


KIUNGO wa Simba, Mghana, James Kotei, jana Jumapili alivamia mazoezi ya Yanga ya asubuhi katika gym iliyopo kwenye Jengo la City Mall, Posta jijini Dar es Salaam.

Kotei ambaye hivi karibuni aliongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Simba, kabla ya kusaini mkataba huo alikuwa akihusishwa na Yanga jambo ambalo liliwafanya Simba kufanya haraka kumuongezea mkataba.

Yanga ambayo ilianza mazoezi ya gym Jumatano iliyopita, imekuwa ikifanya hapo siku zote na jana Jumapili baadhi ya wachezaji wa timu hiyo walikwenda kwa ajili ya kufanyiwa vipimo mbalimbali.

Championi Jumatatu ambalo lilikuwepo hapo tangu saa 1:30 asubuhi, lilianza kuwashuhudia wachezaji wa Yanga wakiingia mmojammoja, kisha baadaye meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh pamoja na daktari, Edward Bavu, nao wakaingia.

Ilipofika saa 3:01 wakati wachezaji wa Yanga wakiwa ndani ya gym hiyo, ghafla akaingia Kotei na kuanza kufanya mazoezi mwenyewe.

Kotei aliliambia Championi: “Nimeamua kuja kujiweka fiti lakini siyo mpenzi sana wa masuala ya gym, sijajisajili na gym hii, ila naweza kufanya leo hapa, kesho nikaenda sehemu nyingine, kikubwa nataka kujiweka fiti tu kabla ya kuanza kwa msimu ujao.”CHANZO: CHAMPIONI

No comments