Header Ads

Nick Minaj amzimikia mkali wa muziki kutoka Nigeria, WizkidSTAA wa Hip Hop kutoka Marekani, Nicki Minaj amemfagilia mkali wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid baada ya kuingia katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii na kusapoti shoo aliyoifanya. 


Jumapili iliyopita, Wizkid anayebamba na Ngoma ya Come Closer alialikwa katika tamasha jijini Washington, D.C ambapo alipata shangwe za kutosha kwa mashabiki wake. 

Baada ya kumalizika kwa tamasha hilo, Wizkid alitumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru mashabiki wake ambapo katika ‘posti’ 

hiyo, Nicki Minaj alianza kwa ‘ku-like’ na baada ya muda ‘aka-komenti’ kwa kuonesha ishara ya moto. Hii si mara ya kwanza kwa Nicki Minaj kufanya hivyo, alishawahi kuweka wazi kuwa ni mpenzi wa nyimbo za Nigeria. Ikumbukwe pia, Nicki ameshawahi kuposti kava la ngoma mpya ya msanii wa Nigeria, Skales na kumfagilia

No comments