Header Ads

Pepe ameihama Real Madrid leo

Baada ya kuichezea club ya Real Madrid kwa miaka kumi beki wa kati wa kimataifa wa Ureno Kepler Leveran Pepe ameihama rasmi club hiyo na kuamua kujiunga na club ya Besiktas ya Uturuki.

Pepe anaondoka Real Madrid ambayo ameichezea kwa mafanikio katika kipindi cha miaka 10, beki huyo raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 34, alijiunga na Real Madrid ya Hispania mwaka 2007 akitokea FC Porto ya kwa Ureno.

Staa huyo wa Ureno ambaye ameisaidia Ureno kutwaa taji la Euro 2016 anaondoka Real Madrid kama mchezaji huru lakini akiwa na club hiyo katika misimu 10 ameichezea game 334 na kushinda mataji 13, Pepe alisema mapema kuwa hatoendelea na Real Madrid.

No comments