Header Ads

Profesa Jay Afunga Ndoa Kanisa la St. Joseph -Dar (Pichaz + Video)

ProfesaJay Profesa Jay akiwa na mkewe kipenzi, Grace Mgonjo, mara baada ya kufunga ndoa katika kanisa la St. Peters, Mbuyuni jijini Dar
Profesa Jay amefunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu Joseph la Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 08, 2017 na mpenzi wake wa siku nyingi Grace Mgonjo.

Cherekochereko za tukio kubwa la Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule almaarufu Profesa Jay limetikisa Jiji La Dar baada ya kufuatiliwa na watu wengi. Ndoa ya Profesa Jay na mpenzi wake wa muda mrefu. Kabla ya ndoa hiyo iliyoibua shangwe kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofurika kanisani hapo, msafara wa kuelekea kanisani ulianzia nyumbani kwa Profesa Jay, Kimara-Temboni jijini Dar.

Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo waalikwa walipata nafasi ya kula, kunywa hadi kusaza huku shughuli nzima ikipambwa na mahudhurio ya mastaa kibao wa Bongo.
“Namshukuru Mungu nimetimiza ahadi ya ndoa kwa mchumba wangu ambaye tumepitia mabonde na milima,” alisema Profesa Jay baada ya kutoka kanisani hapo.

Profesajay ...Grace akiingia kanisani kwa ajili ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Profesa Jay.profesajay ...Profesa Jay akiwa ameketi na mkewe muda mfupi baada ya kuingia kanisani tayari kwa tukio takatifuMr. II Joseph Mbilinyi 'Mr II' (kulia), ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema, akiwa kanisani wakifuatilia ibada ya ndoa.Profesajay ...wakipewa mkono wa dua mara wakati wakikamilisha tendo la Ibada ya Ndoa.Profesajay .....wakila kiapo cha ndoa mbele ya padri na mashahidi..."Mungu tusaidie'..Ameenprofesajay ...Grace akipewa mkono wa pongezi na baraka mara baada ya kufunga ndoa.ProfesaJay ....Wakiwa na nyuso za tabasamu na furaha tele mara baada ya kukamilisha tendo takatifu la ndoaProfesajay ....wakionesha vyeti vya ndoa yao mara baada ya kuvisaini na kukabidhiwa.Prosejajay  
....akiwa na Best Man wake muda mfupi kabla ya kuingia kanisani.

 
A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on
 
A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on
PICHA NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERSNo comments