Header Ads

Said Mrisho Aliyetobolewa Macho na Scorpion Adaiwa Kufumaniwa!

Said Mrisho (katikati) akiwa na familia yake.

SAID Mrisho, yule kijana aliyedaiwa kutobolewa macho na mtu anayetambulishwa kwa jina la Salum Njwete ‘Scorpion’, baada ya kudaiwa kumtelekeza mke na watoto, amekwaa balaa jingine ambapo awamu hii amedaiwa kufumaniwa na mkewe wa ndoa, Stara Soud  tukio lililozua varangati la kufunga mtaa, twende aya kwa aya.
Kwa mujibu wa maelezo yenye ujazo wa kilo na tani kutoka kwa mkewe, sokomoko hilo linalozua na kuammsha hisia tofauti, lilijiri Jumapili ya wiki iliyopita maeneo ya Tabata kufuatia kunasa sauti ya mumewe kupitia simu ya mkononi aliyokuwa akizungumza naye siku moja kabla, ambapo alimdanganya kuwa anasafiri kwenda mkoani Mtwara kikazi.

KUNA HAYA MAELEZO KWANZA
Kwa muda mrefu tangu Said akumbwe na tatizo la kutobolewa macho, amekuwa akiishi ukweni kwao, yaani nyumbani kwa mke wake maeneo ya Mabibo-Hosteli akiuguzwa kwa ujalifu na uangalifu wa hali ya juu hadi alipopata unafuu, ambapo siku zote hizo, familia ya wakwe zake walilazimika kusitisha shughuli mbalimbali na kujikita kumuuguza ambapo ndugu zake hawakuwa na ushirikiano huo.Stara Soud na watoto wake.

MAZINGIRA YA FUMANIZI SASA
Said alipopata unafuu, ndipo mipango ya kuondoka nyumbani hapo kwenda kupanga sehemu nyingine ilianza kufanyika, ambapo walipata nyumba maeneo ya Tabata-Kisukulu na kuanza kuhamishia baadhi ya vitu baada ya kuwa wamekwishalipia kila kitu, lakini ghafla Said alibadili uamuzi na kumueleza mkewe kuwa ameona kodi ya Tabata ni kubwa mno hivyo amerudishiwa kodi yake na ameamua kupanga nyumba maeneo ya Ubungo Majichumvi, jambo ambalo mkewe aliliunga mkono lakini baadhi ya vitu vilibaki kule Tabata.

SIKU YA FUMANIZI
“Tulihamia kule Majichumvi, lakini siku hiyo alisema anasafiri kwenda Mtwara na kunitaka nimuandfalie nguo, kweli alirudi jioni sana na kunikuta napanga baadhi ya vitu, akasema atakwenda kulala kwa rafiki yake ili awahi kuondoka, usiku akanipigia simu na kunitaarifu kuwa kuna mahali amekaa anakula, baada ya mazungumzo kumbe hakukata simu na nikamsikia akimwambia mtu kuwa amenidanganya amesafiri na kwamba ataniacha taratibu na mwisho wa siku atakuwa huru.

“Niliumia sana, nikampigia simu mama na kesho yake nikaenda nyumbani hivyo mimi na dada yangu tukaamua kwenda kwenye ile nyumba tuliyolipia awali Tabata, kuhakikisha huenda yuko kule, kweli tukamkuta mwanamke mmoja na tulipombana akasema yeye ni mkewe na Said yumo ndani, tukiwa sebuleni Said alitoka chumbani na kuanza kurusharusha mikono akifanya fujo, bila kujali kuwa nimemfumania, nimeumia sana kwani nimetoka naye mbali, nilipoga makelele ya vilio na watu wakajaa, baadaye tulikwenda polisi ambako tulishauriwa twende ustawi wa jamii kwani kuna suala la watoto na kifamilia,” alisema Stara, mke wa Said.

INASIKITISHA: Aliyetobolewa Macho na Scorpion Amtelekeza Mke, Watoto… Mkewe aanika Mazito

No comments