Header Ads

MTANGAZAJI WA EFM ‘BIKIRA WA KISUKUMA’ AFARIKI

Mtangazaji wa EFM, Seth Katende almaarufu Bikira wa Kisukuma enzi ya uhai wake.
Mtangazaji za kituo cha redio cha EFM, Seith Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Bikira wa Kisukuma (kushoto) akiwa na Dina Marious.[/caption]Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyakazi wenzake ambao hawakutaka kutajwa majina yao kwa vile siyo wasemaji, walisema marehemu alianza kuugua kiasi cha mwezi mmoja uliopita na msiba uko nyumbani kwa baba yake mzazi huko Changanyikeni.
Marehemu ambaye alikuwa akitangaza kipindi cha Ubaoni, kinachorushwa na redio hiyo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa kumi jioni, alikuwa pia ni bloga maarufu katika mitandao ya kijamii.
 

No comments