Header Ads

Video: Rais Magufuli Ametoa Onyo Kali Kwa wanasiasa wa Tanzania

Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wanasiasa, bila kumtaja jina yeyote lakini akionesha zaidi kumlenga aliyekuwa mpinzani wake mkubwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2015, Edward Lowassa.

Hivi karibuni, Lowassa alitoa kauli ya kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kupigania haki za ndugu zao wanaoteseka gerezani.
Muda mfupi baada ya kauli hiyo, Lowassa aliitwa na mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP), ambapo alihojiwa mara mbili mfululizo.


Rais Magufuli, ameshangaa iweze mwanasiasa ajitokeze kutetea watu wanaofanya mambo mabaya, wakati hata Guantanamo watu wabaya hukaa miaka mingi kuliko kawaida.


Akazidi kuhoji iweje mwanasiasa hajawahi kulaani mauaji ya Kibiti hata siku moja lakini anaibuka na kutetea watu waliopo gerezani. Akawataka polisi wawashughulikie vizuri wanasiasa hao, bila kujali sura zao wala mwendo.

No comments