Header Ads

Yanga yamtambulisha rasmi AjibuKLABU ya Yanga, leo imemtambulisha rasmi straika waliyemsajili kutoka Simba, Ibrahim Ajib.

Ajibu amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na ametambulishwa leo Jumatano mbele ya Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani jijini Dar.

Yanga imefanikiwa kuinasa saini ya Ajibu baada ya mchezaji huyo kushindwa kuafikiana na uongozi wa klabu yake ya zamani katika makubaliano ya mkataba mpya.

Ajibu anakuwa mchezaji wa tatu kusajili na kutambulishwa na Yanga katika kipindi hiki baada ya awali klabu hiyo kumsajili beki wa Taifa Jang’ombe, Abdallah Haji ‘Ninja’ na kiungo wa Mbao FC, Pius Buswita.

Mbali na usajili wa wachezaji hao wapya, pia tayari imeshawaongezea mikataba mastraika wao wawili hatari, Mzimbabwe, Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe.

No comments